Jinsi ya kupika pilau ya njegere
Mahitaji
- 250 gram mchele wa basmati
- 1 kijiko binzali nyembamba (cumin seeds)
- 1/2 kijiko kidogo cha chai garam masala
- 1/2 kijiko kidogo cha chai coriander powder
- 1/4 kijiko kidogo cha chai turmeric powder
- 60 gram njegere za kuchemshwa
- 1 kitunguu maji chop chop
- 3 nyanya za kuiva nazo chop chop
- 1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya kusagwa
- 1kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa
- 2 pili pili mbuzi, kisha kata vipande vidogo vidogo
- 60 gram korosho au karanga za kukaanga (sio lazima)
- 1 kijiko kidogo cha chai siagi au mafuta ya samli kwa ladhamajani ya giligilani na majani ya mint kwa kupambia na kuongeza ladha
Jinsi ya kupika
- Weka kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia kwenye kikaango kama ni samli au siagi, kisha garam masala, unga wa manjano, binzali nyembamba na unga wa corienda kaanga kidogo kisha weka kitunguu swaumu, kitunguu maji, tangawizi, pilipili mbuzi na nyanya zote ziwe chop chop vipande vidogo kama inavyoonekana kweny picha. Kisha weka chumvi, karafuu na pili pili manga endelea kukaanga.
- Ukishapata harufu ya kunukia na mboga zako ziwe zimeanza kuiva basi mimina mchele na endelea kukaanga wali wako huku ukiuchanganya uchanganyike vizuri kabisa na mboga kwa dakika 2 au 3. .
- Weka gram 600 za maji kisha koroga na funika na mfuniko acha iive kwa dakika 10 kwa moto wa wastani.
- Baada ya dakika 10 itakua imekaribia kabisa kuiva, kisha weka njegere zilizoiva na koroga kidogo ichanganyike kisha pika kwa dakika 2 tena.
- Baada ya pilau yako kuiva basi juu yake weka majani ya mint au giligilani kuongeza uzuri wa rangi, ladha na harufu safi sana katika pilau yako.
- pia ukiwa mpenzi wa siagi weka kwa juu kiasi au unaweza mwagia samli hii nikuongeza harufu nzuri na ladha zaidi.
- Usisahau kuweka karanga au korosho za kukaanga kwa juu.
Maji gram 600 yanakuaje na nitayapata wapi
ReplyDelete