TAMBI ZA MAYAI

MAHITAJI

Tambi ½ kg
MAYAI 4
Sukari kiasi
Chumvi
Maji 1lita
Vanilla au unga wa hiliki ½ kijiko cha chai.
Nyanya 3,
Karoti 1 kubwa
Pilipili hoho 1
KItunguu maji1
Namna ya kupika
Chukua maji na kisha weka chumvi kiasi cha nusu kijiko cha chai, injika maji jikoni na kisha yaache yachemke, weka tambi zako katika maji hayo acha zichemke kwa muda wa dakika tano.
Katakata kitungu maji kisha kikaange kikishaiva weka hoho,karoti, nyanya, vichemshe kwa dakika tano kisha weka mayai, changanya mchanganyiko wako vizuri.
Baada ya hapo chukua hizo tambi na ziche maji yote na kisha miminia katika mchanganyiko wa mayai na changanya vizuri, weka sukari kiasi unachohitaji na mwisho weka vanilla au hiliki na kisha funika. acha vichemke kwa dadika tatu, halafu epua
tambi zako zipo tayari kwa kuliwa..

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kupika pilau ya njegere

JINSI YA KUPIKA BIRINGANYA

CHICKEN MASALA