Posts

Showing posts from September, 2017

MAGAZETI YA LEO SEPT 13 2017

Image

Minofu ya kuku ya kukaanga

Image
  Mahitaji 500g/ nusu kg minofu ya kuku Vikombe 2 vya chai chenga za mkate (Bread crumbs) Vijiko 3 vya chakula unga wa ngano Mayai 2 Kijiko 1 cha chakula tangawizi na kitunguu saumu Chumvi na pilipili manga kwa kuonja Mafuta ya kukaangia Maelekezo Osha, kausha na katakata minofu ya kuku vipande virefu vyembamba kiasi Kwenye bakuli kubwa, Changanya vizuri vipande vya kuku tangawizi na kitunguu saumu; chumvi na pilipili manga. Weka pembeni Chemsha mafuta kwenye kikaangio moto wa juu kiasi. Wakati mafuta yanachemka, piga yai kwenye bakuli Paka vipande vya kuku unga wa ngano, halafu chovya kwenye yai lililopigwa na mwishoni zungushia kuku wako chenga za mkate. Kwa kutumia mkono, gandamiza chenga kwenye kuku zishike vizuri Weka kuku kwenye mafuta yaliyochemka, acha aive hadi awe na rangi ya kahawia na mkavu kwa juu. Unaweza kuongeza na kupunguza moto ikibidi Kuku akiiva, weka kwenye sahani yenye tissues za jikoni kukausha mafuta Enjoy

Chapati za kumimina zenye oatmeal

Image
Chapati za kumimina zenye  oatmeal 1/3 kikombe unga wa ngano 1/3 kikombe Oatmeal Mayai 2 1/4 kijiko cha chai chumvi Kijiko 1 cha chakula sukari Kikombe 1 maziwa Siagi kwa ajili ya kukaangia Filling Nutella kiasi chako Ndizi mbivu 1 iliyokatwakatwa Maelekezo Weka oatmeal kwenye mashine ya kusagia chakula, saga ilainike iwe unga Kwenye bakuli kubwa koroga maziwa,  mayai,  chumvi na sukari mpaka ichanganyike vizuri Ongeza unga wa ngano na oatmeal iliyosagwa. Changanya vizuri Funika, hifadhi kwenye jokofu siyo chini ya dakika 30 Kwenye kikaango ambacho hakishiki chini katika moto wa wastani, weka robo kikombe unga. Kwa haraka, sambaza vizuri mchanganyiko wako usambae kikaango kizima. Acha ipike hadi kona zionekane zina rangi ya kahawia kiasi Kwa kutumia kijiko kipana,  geuza chapati upande wa pili, paka siagi upande uliopika Pika na upande wa chini uive uwe na rangi ya kahawia pia kisha geuza upake siagi. Geuza tena pande zote mpaka iive vizur

WALI WA KUKAANGA

Image
MAHITAJI Kwa wali na mbogamboja Vikombe 2 wali uliopikwa Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu Kitunguu maji 1 cha wastani Karoti 1 Kikombe 1 maharagwe machanga Kitunguu cha majani Kwa sosi Vijiko 2 vya chakula sosi ya soya Kijiko 1 cha chakula mafuta ya ufuza (Ukipenda) Kijiko 1 cha chai tangawizi (ukipenda) Mbegu za ufuta (ukipenda) Maelekezo maji. Pika kwa dakikaAndaa viungo; katakata maharagwe, karoti, majani ya kitunguu na kitunguu maji vipande vidogovidogo sana; Twanga kitunguu saumu na tangawizi, weka pembeni Kwenye kikaangio kikubwa katika moto wa juu kiasi, chemsha mafuta. Ongeza kitunguu saumu mpaka kiive, halafu uongeze kitunguu maji. Pika mpaka kiive Ongeza karoti na maharagwe machanga. Pika mpaka viive kama utakavyopenda wewe Ongeza wali changanya vizuri Changanya sosi ya soya, mafuta ya ufuta na tangawizi kwenye bakuli, weka pembeni. Ongeza mchanganyiko wa sosi na kitunguu cha nyingine 1, ipua Pa

CHIPS ZA NDIZI MZUZU

Image
  Mahitaji Ndizi mzuzu tatu kubwa Vijiko 4 vya chakula chenga za mkate Mafuta ya kutosha ya kukaangia Chumvi au viungo vingine Maelekezo Menya na kukatakata ndizi umbo la chispi kubwa kubwa kiasi; nyunyizia chumvi na pilipili manga uchanganye vizuri Kwenye kikaangio kikubwa moto wa juu kiasi, weka mafuta ya kupikia acha yachemke vizuri. Wakati mafuta yanachemka, chovya vipande vya ndizi kwenye chenga za mkate hadi zifunikwe vizuri, kandamiza na mkono chenga zishike kwenye ndizi vizuri Kaanga kwa dakika mbili upande wa kwanza, geuza kwa dakika moja upande wa pili, au mpaka ziive ziwe na rangi ya kahawia Ipua kutoka kwenye mafuta, ziweke kwenye sahani yenye tissues zichuje mafuta Enjoy

Mapishi ya Sambusa Za Nyama /Jinsi ya kupika sambusa hatua kwa hatua

Image
    Mapishi ya Sambusa Za Nyama /Jinsi ya kupika sambusa hatua kwa hatua Mahitaji ½ kilo Nyama ya iliyosagwa kijiko 1 kikubwa cha chakula cha Pilipili manga Kijiko kimoja cha chakula cha kitunguu Thomu na tangawizi iliyosagwa Mafuta ya kupikia Kiasi Vijiko vinne unga ngano au ute wa yai kwa kufungia sambusa Kaki za sambusa/manda/ chapati nyepesi (unaweza kununua zilizokuwa tayari zimeshakatwa kwa ajili ya sambusa au kama utanunua zile sheet pana utazikata kwa inchi 4 upana wa ruler yaani upate mistari 3 Directions Kausha nyama ya kusaga kwa kiyunguu swaumu (thomu) na tangawizi pamoja na chumvi mpaka ikauke vizuri Iwache ipoe. Kata kata majani ya kotmiri weka upande Kata kata upate vipande vidogo vidogo(chop) vya vitunguu maji. Zikate pili pili zako slice za mviringo vidogo vidogo. Wakati ukimaliza matayarisho haya na nyama yako itakuwa ishapoa kabisa hapo ndio utachanganya,bizari nzima pamoja na pilipili manga pamoja na vitu vyote ulivyokwisha vitaya

Makubwa ya Magazeti ya TZ leo September 12

Image
Makubwa ya Magazeti ya TZ leo September 12.. Udaku, Michezo na Hardnews September 12, 20

CHICKEN MASALA

Image
CHICKEN MASALA Viungo Majani 2-4 ya bay ( Bay leaves ; kutegemea na ukubwa) Anise star 1 Iliki nzima 4 Karafuu punje 5 Vijiti 1-2 vya mdalasini Kijiko 1 cha chai garam masala Vijiko 2 vya chai chicken bouillon powder ½ kijiko cha chai coriander ½ kijiko cha chai binzari ya pilau ½ kijiko cha chai pilipili ya kukausha ½ kijiko cha chai binzari ya manjano Chumvi kwa kuonja ikihitajika Osha, kausha na kuchanja kuku Twanga kitunguu saumu na tangawizi; kamua maji limao na katakata majani ya giligilani Kwenye bakuli kubwa, weka kuku, maji ya limao, kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu, kijiko 1 cha chakula tangawizi, chumvi na vijiko 2 vya chakula mafuta Changanya vizuri, funika na hifadhi kwenye jokofu kwa masaa si chini ya 2 Kwenye kikaango katika moto wa juu kiasi, chemsha vijiko 3 vya mafuta. Ongeza kuku, kanga kila upande kwa dakika kama 2 hadi 3; au mpaka rangi ya ngozi iwe kahawia kiasi, isikauke sana. Ipua, weka pembeni Weka nyanya, k

Supu Ya Brokoli (Broccoli)

Image
Supu Ya Brokoli (Broccoli) Supu Ya Brokoli (Broccoli) Vipimo Brokoli - 1 msongo (bunch) Parlsely - 3 misongo Karoti - 2 Viazi - 2 Vitunguu - 1 – 2 Nyanya - 1 Kidonge cha supu (stock/ Maggi cube) - 1 Pilipili manga - 1 kijiko cha chai Chumvi - kiasi Ndimu - 1 kijiko cha chai Mafuta - 2 kijiko cha supu Zaytuni - kiasi Namna ya kutayarisha na kupika Chambua brokoli, katakata karoti, viazi, vitunguu na nyanya. Chemsha brokoli, karoti na viazi. Tia mafuta katika sufuria kaanga vitunguu hadi vilainike, tia nyanya, endelea kukaanga. Tia pilipilimanga, chumvi na kidonge cha supu. Mimina vitu ulivyochemsha na supu yake katika mkaango. Tia katika mashine ya kusagia (blender). Tia parselye usage kidogo tu, kisha rudisha katika sufuria urejeshe katika moto na ipike kidogo kwa muda wa 1 tu. Onja chumvi, ndimu ikiwa tayari kuliwa pekee au na mkat

Jinsi ya kupika pilau ya njegere

Image
​ Jinsi ya kupika pilau ya njegere Mahitaji 250 gram mchele wa basmati 1 kijiko binzali nyembamba (cumin seeds) 1/2 kijiko kidogo cha chai garam masala 1/2 kijiko kidogo cha chai coriander powder 1/4 kijiko kidogo cha chai turmeric powder 60 gram njegere za kuchemshwa 1 kitunguu maji chop chop 3 nyanya za kuiva nazo chop chop 1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya kusagwa 1kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa 2 pili pili mbuzi, kisha kata vipande vidogo vidogo 60 gram korosho au karanga za kukaanga (sio lazima) 1 kijiko kidogo cha chai siagi au mafuta ya samli kwa ladhamajani ya giligilani na majani ya mint kwa kupambia na kuongeza ladha Jinsi ya kupika Weka kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia kwenye kikaango kama ni samli au siagi, kisha garam masala, unga wa manjano, binzali nyembamba na unga wa corienda kaanga kidogo kisha weka kitunguu swaumu, kitunguu maji, tangawizi, pilipili mbuzi na nyanya zote ziwe chop chop vipande

Jinsi ya kupika wali wa manjano

Image
​ Jinsi ya kupika wali wa manjano Mahitaji 1 au 2 Saffron ( zafarani ya orange) 4 kijiko kikubwa cha chakula Olive oil 1 kitunguu kikubwa kata kata 1 pili pli hoho katak kata vipande vidogo vidogo 1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kupondwa 240 gram mchele wa basmati 340 ml za maji ya vugu vugu 5 gram ya chumvi Majani kiasi ya giligilani kwa ajili kupambia na kuongeza ladha Jinsi ya kupika Washa jiko lako katika moto mdogo, weka kikaango chako kwenye moto kisha weka mafuta, kitunguu maji na safron pamoja na endelea kukaanga pole pole. Baada ya mafuta kubadilika rangi ya machungwa yatoe katika moto na acha ipoe kwa dakika 10 kisha yachuje hayo mafuta. Chukua kijiko kimoja kikubwa cha mafuta na weka katika kikaango. Kisha chukua tena kitunguu maji na kitunguu swaumu endelea kukaanga mpaka vilainike. Kisha ongeza pili pli hoho na endelea kukaanga mpaka iwe laini. Kisha weka mchele na endelea kukaanga pole pole mpaka mchele utaponukia na kubadilika

TAMBI ZA KUPALIA

Image
  Tambi za kupalia Mahitaji Tambi ½ kg Maji lita 1 Chumvi kiasi Tui bubu la nazi kikombe 1 cha chai Sukari kiasi Namna ya kupika Chukua maji yaweke jikoni na kisha weka chumvi 1/2 kijiko cha chai, acha maji yachemke na kisha weka tambi acha zichemke kwa muda wa dakikia tano zitakuwa zinakaribia kuiva. Baada ya kuhakikisha kuwa zinakaribia kuiva zichuje maji yote na kisha weka tui la nazi sukari na unga wa hiliki. Acha maji yakauke kabisa na kisha palia mkaa au weka kwenye oven kama unavyofanya kwa wali. Baada ya dakika kumi tambi zako zitakuwa ziko tayari kwa kuliwa. Futari hizi kwa kawaida huliwa kwa na uji au chai

TAMBI ZA MAYAI

Image
MAHITAJI Tambi ½ kg MAYAI 4 Sukari kiasi Chumvi Maji 1lita Vanilla au unga wa hiliki ½ kijiko cha chai. Nyanya 3, Karoti 1 kubwa Pilipili hoho 1 KItunguu maji1 Namna ya kupika Chukua maji na kisha weka chumvi kiasi cha nusu kijiko cha chai, injika maji jikoni na kisha yaache yachemke, weka tambi zako katika maji hayo acha zichemke kwa muda wa dakika tano. Katakata kitungu maji kisha kikaange kikishaiva weka hoho,karoti, nyanya, vichemshe kwa dakika tano kisha weka mayai, changanya mchanganyiko wako vizuri. Baada ya hapo chukua hizo tambi na ziche maji yote na kisha miminia katika mchanganyiko wa mayai na changanya vizuri, weka sukari kiasi unachohitaji na mwisho weka vanilla au hiliki na kisha funika. acha vichemke kwa dadika tatu, halafu epua tambi zako zipo tayari kwa kuliwa..

JINSI YA KUPIKA BIRINGANYA

Image
MAHITAJI 1.biringanya, karoti, pilipili hoho, nyanya, chumvi, pilipili, tomato paste, nazi, green beans, kitunguu maji, mafuta ya mboga, pilipili manga, binzari nyembemba, JINSI YA KUPIKA  M enya biringanya kisha likate vipande vidogo vidogo, tayarisha viungo vyako (nyanya, karoti,hoho,green beans, kitunguu maji.) injika sufuria jikoni, kaanga kitungu kikishaiva weka biringanya pamoja na green beans na chumvi, funika kwa muda kisha weka mchanganyiko wa mboga mboga na viungo. funika kwa muda wa dakika 10, kisha  weka tomato paste na nazi changanya vizuri acha vichemke kwa dakika kadhaa kisha tegua. mchanganyiko wako uko tayari kwa kuliwa. unaweza kula na wali, ugali, tambi,  na chapati

MAKANGE YA KUKU

Image
 JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA KUKU mkate kuku vipande, andaa vituguu maji, chumvi,mafuta, nazi, nyanya na maji. chemsha mafuta kidogo yakisha chemka tia nyama yako ikichemka na kubadilika rangi weka vitunguu, karoti kisha nyanya na chumvi. mchanganyiko ukikolea na kuku wako kuiva tia tui la nazi na usifunike. baada ya nusu saa makange yatakakua tayari